Duration 9:31

RcSingida Dkt. Binilith Mahenge Awataka Watendaji wa Serikali Kuvilinda Vyanzo vya Mapato.

255 watched
0
1
Published 10 Jun 2021

MKUUwa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kusimamia ipasavyo vyanzo vya mapato vilivyopo kwenye maeneo yao ili kutovipoteza kufanya makusanjo yaongezeke. Mahenge alitoa agizo hilo leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani hapa akiwa katika muendelezo wa ziara yake za kutembelea halmashauri zote kwa ajili ya kukagua Miradi ya maendeleo na kuzungumza na Watumishi, watendaji na wananchi. Mahenge Amesema anataka viongozi hao hasa watendaji kujua kuwa kupata mapato kunafanywa na Umoja na Mshikamano baina ya Wakuu wa Idara na Mkurugenzi bila kuwaacha Madiwani. Dkt Mahenge amewataka Madiwani kufuatilia kwa karibu ukusanyaji wa Mapato ili wanapo kaa kwenye Baraza wajue Mapato halisi yaliyotokana na Kata yake.

Category

Show more

Comments - 0