Duration 9:6

WANAFUNZI KOZI YA MAENDELEO YA JAMII SUA CDA NA CRDB WAUNGANA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

148 watched
0
1
Published 17 Jun 2021

Wanafunzi wa kozi ya Maendeleo ya Jamii SUA (CDA) kwa kushirikiana na Benk ya CRDB tawi la SUA wameungana kwa pamoja kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika. Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kwa nchi zote za Afrika kwa lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto kwa jamii na Taifa kwa ujumla. Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi ya mtoto wa Afrika mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika baada ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea Soweto Afrika ya kusini na kupelekea watoto zaidi ya 2000 kupoteza maisha hivyo Umoja wa Afrika ukaona umuhimu wa kutenga Siku hii kuwa Siku ya Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika. Maadhimisho ya Siku ya mtoto wa Afrika kwa mwaka wa 2021 yalibebwa na kaulimbiu isemayo "Utekelezaji Ajenda 2040 inayolinda haki za Watoto".

Category

Show more

Comments - 0