Duration 5:42

LIVE​: Tazama Ziara ya Waziri wa Ulinzi na JKT Dkt Stergomena Tax Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu

36 310 watched
0
149
Published 12 Oct 2021

Waziri wa Ulinzi na JKT Mheshimiwa Dkt Stergomena Lawrence Tax ametembelea Makao Makuu ya Kamandi ya Jeahi la Nchi Kavu (Land Force Command) iliyoko Msangani Mkoa wa Pwani. Hii ni ziara ya kwanza kwa Mheshimiwa Waziri Tax kuitembelea Kamandi hio tangu alipoteuliwa na kuapishwa kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT. Mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu alipokelewa na kupata taarifa fupi (Briefing) iliyoambatana na Mafanikio ya kiutendaji yalifikiwa na Jeshi kupitia Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu, Aidha Changamoto kadhaa nazo ziliainishwa mbele ya Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na JKT ambapo aliahidi kuzitafutia ufumbuzi na Kuzitatua, Pamoja mambo mengine mengi Mheshimiwa Waziri alitembezwa na kujionea maonesho kadhaa ya kiutendaji ambapo alifurahishwa mno na ARI, WELEDI na MOYO WA KUJITUMA kwa Makamanda wakuu, Maofisa na Askari katika kutekeleza Majukumu yao.

Category

Show more

Comments - 32