Duration 4:18

Rais Magufuli apiga msumali wa mwisho sakata la makontena ya RC Makonda

119 091 watched
0
357
Published 30 Aug 2018

Rais Magufuli hatimaye amekata mzizi wa fitna kuhusiana na makontena Ishirini yanayoshikiliwa Bandarini Jijini Dar Es Salaam yakidaiwa kuwa na samani za shule yaliyoletwa kwa msaada kwa jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda akisema ni lazima yalipiwe kodi. Dokta Magufuli amesema kwamba makontena hayo yanayodaiwa kodi yenye thamani ya Bilioni Moja Nukta Mbili yanapaswa kulipiwa kodi hiyo kwa sababu aliyeletewa hana mamlaka ya kisheria ya kupata msamaha huku pia akihoji ni kwa nini shule zinazopelekewa samani hizo hazijatajwa. Rais Dokta Magufuli amezungumza hayo akiwa Chato Mkoani Geita alipokutana kwa mazungumzo na Viongozi na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

Category

Show more

Comments - 38